Mazungumzo Magumu na Tundu Lissu
Mgombea uraisi kwa tiketi ya Chadema, Ndugu Tundu Lissu alifanya mahojiano na BBC kupitia kipindi chao cha Hard Talk yani Mazungumzo Magumu. Mahojiano hayo yalifanywa na mtangazaji Stephen Sackur na kipindi kilirushwa siku ya Jumatatu, 21 Januari 2019. Video ya mahojiano hayo yana patikana Youtube.
Mahojiano kati ya Bwana Sackur na Bwana Lissu yalichukua takribani dakika 23. Mazungumzo hayo yalijikita kwenye mada kuu tatu ambazo ni shutuma za Tundu Lissu juu ya walio husika na shambulio lake September 2017, utendaji kazi wa raisi Magufuli haswa kwenye kupambana dhidi ya rushwa na mikataba mibovu ya madini na mwisho msimamo wa Tundu Lissu kuhusu swala la ushoga na sheria zinazo pingana na vitendo hivyo.
Swali la kwanza kabisa analo ulizwa Lissu ni juu ya madai yake kwamba shambulio lake lilikua la kisiasa na ni serikali iliobariki shambulizi hilo. Shackur aanamuuliza moja kwa moja Lissu kua ushahidi wake ni upi. Lissu anaanza kujieleza kwa kusema kua wiki sita kabla ya shambulizi hilo kuna gari lililo kua linamfuata kila sehemu. Shackur anamhoji hao hawawezi kua watu wowote wale kwa vile alisha wahi kua Raisi wa Tanganyika Law Society na kwamba yaweza ikawa alikua na maadui wengi waliotaka kumdhuru? Lissu akaendelea kutoa shutuma bila kutoa ushahidi wa moja kwa moja. Shackur anambana kwa kumhoji kua anatoa shutuma nzito dhidi ya serikali pasipo na ushahidi wa kueleweka. Ikumbukwe haya ni mahojiano na kituo cha habari cha nje ambavyo ndivyo Ndugu Lissu anavyo vipenda siku hizi.
Swala la pili ni kuhusu Raisi Magufuli alivyo pambana na rushwa na mikataba mibovu ambayo nchi ilikua imeingia huko nyuma. Sackur akataja mifano kama vile kuondolewan kwa wafanyakazi hewa kwenye malipo ya serikali, kufukuzwa kwa vigogo katika mamlaka ya bandari TPA na mamlaka ya mapato TRA na pia mpambano kati ya serikali na kampuni ya Barick Gold. Sackur akaenda mbali zaidi na kusema mafanikio haya dhidi ya rushwa ni jambo la kupongezwa haswa katika nchi za Kiafrika. Lissu akakwepa kujibu hoja hii na akajikita zaidi kumtuhumu Raisi kwa kununua ndege kwa ajili ya Air Tanzania na kudai hio sio kazi ya raisi. Ikafika kipindi Sackur akatamka wazi kua ni kama vile Lissu hafurahii kitendo cha raisi kupambana na makampuni ya kigeni tulio ingia nao mikataba mibovu na ni kama vile Lissu yuko upande wa hayo makampuni.
Kwenye hili swala la pili pia aliulizwa kuhusu viongozi mbalimbali wa upinzani kuhama na kujiunga na CCM ili kuunga juhudu za Raisi Magufuli. Lissu kwa mara nyingine akatoa shutuma za kwamba viongozi hao wa upinzani walinunuliwa. Sackur akamtatisha na kumuuliza Lissu yeye kama mwanasheria inampasa awe muangalifu kutoa shutuma pasipo kutoa ushahidi wowote. Lissu akakaa kimya.
La mwisho ni swala la sheria kuhusiana na vitendo vya ushoga nchini na adhabu ya miaka 30 kwa mtu atakae hukumiwa kwa vitendo hivyo. Sackur akamuuliza swali la moja kwa moja la je yupo tayari kusema mbele ya ulimwengu kua kama atakua raisi atafuta sheria zinazo husiana na ushoga? Baada ya kuzunguuka swali na kukwepa kujibu akaulizwa tena kwa mara ya pili, je yupo tayari kufuta sheria hizo iwapo atapewa madaraka ya uraisi? Hatimai Lissu akajibu kua ana amini sheria hizo zinaingilia uhuru binafsi wa mtu na kwamba sheria hizo ni kinyume ya katiba ya Tanzania. Haya ni maneno yake mwenyewe. Yapaswa vyombo vya habari vya Tanzania kumuuliza swali hili hili akiwa sasa yupo nchini kama bado ana mpango wa kufuta sheria hizi dhidi ya ushoga iwapo atafanikiwa kupewa ridhaa ya kuongoza nchi.
Ni rai yangu kwa wasomaji wote wa nakala hii waenda Youtube na kutazama mahojiano hayo mwanzo mpaka mwisho. Haswa kwenye hilo swala la ushoga tumhoji ili iwekwe kwenye rekodi. Asije akawa anazungumza haya akiongea na vyombo vya habari vya magharibi na kisha kuzungumza mengine akiwa anatafuta kura za Watanzania. Pia Lissu ahojiwe ni kweli yuko upande wa makampuni ya kigeni ambayo yamekua yaki nyonya nchi yetu kwa miaka mingi? Je ana amini ilikua kosa serikali kuvunja hii mikataba na kuingia mikataba mipya na rafiki zaidi? Je yeye angekua ndio raisi ange acha makampuni hayo yaendelee kutonyonya?
October Watanzania tunaenda kupiga kura na mwisho wa mwezi huu kampeni zitaanza. Ndugu Lissu yapaswa aulizwe maswali magumu na asionewe huruma kwenye kuhojiwa maswala mazito kwa vile tu alishambuliwa kwa risasi huko nyuma. Hatuja wahi muingiza mtu Ikulu kwa kumuonea huruma na kumpa fadhila kwa yaliyo msibu huko nyuma. Tunampa mtu uraisi kutokana na sera za chama chake na maono yake binafsi. Kabla hajaomba mdahalo na Raisi Magufuli hebu ahojiwe na aulizwe maswali magumu na Watanzania. Its time Tanzanians have a Hard Talk with Tundu Lissu!
Thomas Joel Kibwana