Thomas Joel Kibwana
3 min readJun 19, 2020

Kwa nini Dk. Mwinyi Ndio Chaguo Sahihi.

Tarehe 17 Juni, 2020, Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi alitangaza nia yake ya kuwania uraisi wa Zanzibar. Kwa sisi wafuatiliaji wa kina wa maswala ya siasa ni japo tulilo kua tukitegemea angefanya na asingekua amekitendea haki kipawa chake kama asinge tia nia. Kama atashinda adhma yake ya kua raisi iko mikononi mwa CCM na hatimae Wazanzibari wenyewe. Ila, hizi hapa ndio sababu zangu ya kwa nini chama kimpe kijiti cha kugombea na kwa nini Wazanzibari wana paswa kumchagua.

Kwanza kabisa tuangalie wasifu wake. Dk. Hussein Mwinyi kazalia 23 Disemba, 1966 na akapata shahada yake ya udaktari kwenye chuo cha Marmana na kisha kupata stashahada ya udaktati kwenye chuo cha Hammersmith. Alitibia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kuanzia 1997 mpaka 1998 kisha akafundisha katika hospitali ya kumbukumbu ya Hubert Kairuki kuanzia 1999 mpaka 2000. Zanzibar inafahamika kihistoria kutoa viongozi mashuhuru toka nyanza ya ukdaktari. Kuanzia Dk. Omari Ali Juma, mpaka Dk. Ghalib Bilal, mpaka Dk. Mohammed Shein na Dk. Hussein Mwinyi anakua muendelezo tu wa historia hiyo.

Akiwa na miaka 53, Dk. Hussein Mwinyi kashakua mbunge kwa miaka 20 na waziri kwa idadi hio hio ya miaka. Amesha tumikia kama naibu waziri wa afya, waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Raisi- Muungano, na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taica kuanzia 2010 mpaka hivi sasa. Kuanzia mwanzo Hussein Mwinyi ameaminiwa na wizara zilizo nyeti kwa maslahi ya Watanzania na taifa. Kuaminiwa kuwa waziri wa wizara nyeti kama ya ulinzi kwa miaka 10 mfululizo chini ya maraisi wawili ni ishara ya uchapakazi, upeo na kuaminika kwake na taifa kufanya kazi kwa maslahi mapana ya nchi.

Hivyo basi, ni wazi Dk. Hussein Mwinyi anayo elimu na uzoefu wa kisiasa wa kushika ofisi kuu ya umma ya Zanzibar. Upeo wake wa kisiasa na uzoefu wake uta hakikisha Wazanzibari wanakua na raisi ambae hata hitaji mafunzo ya kazi na ambae atakua tayari kubeba majukumu ya ofisi hio kuanzia siku ya kwanza. Ila, naamini uraisi wake hautakua na manufaa tu kwa Zanzibar bali na kwa Tanzania kiujumla. Moja kwa moja raisi wa Zanzibar anakua mmoja wa washauri wakuu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na itakua faraja kubwa kua na mtu asie na makuu, mfikiriaji na mwenye upeo mkubwa wa kufikiri kama mshauri mkuu wa raisi kwenye maswala ya muungano.

Sote tunajua muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ume pitia changamoto zake. Dk. Hussein Mwinyi anatoka kwenye historia ya kulinda na kutetea muungano kama vile baba ake alivyo utetea muungano miaka ya tisini wakati halinya muungano ulikua jambo la mjadala mkubwa kitaifa. Sina shaka Dk. Mwinyi ana nia na uwezo wa kuendeleza amani na utulivu na kuongeza ukuaji wa uchumi wa Zanzibar huko akiendeleza udugu wa kisiasa, kijamii na kiuchumi baina ya watu wa Zanzibar na wale wa Tanganyika

Baada ya kusema hayo, naunga mkono kwa moyo wote ugombeaji uraisi wa Dk. Hussein Mwinyi. Dk. Mwinyi yuko tayari na sifa zake hazipingiki. Nilicho furahi zaidi kuhusu yeye ni kwamba hakuchukua njia za mkato na akakubali kupata uzoefu unao hitajika. Hajawahi hata siku moja kuchezea karata ya kua mtoto wa raisi mstaafu wa Zanzibar na raisi wa awamu ya pili. Kila umuonapo kwenye hadhara yupo kama kiongozi na ana muonekano na sauti ya uraisi. Nasubiria kwa shauku kubwa uteuzi wake na halkadhalika uchaguzi wake kama raisi na natangaza hadharani kumuunga mkono kwa moyo mmoja.

Thomas J. Kibwana.

Thomas Joel Kibwana
Thomas Joel Kibwana

Written by Thomas Joel Kibwana

Political enthusiast. International Relations graduate. A fan of everything Tanzania.

No responses yet