Thomas Joel Kibwana
2 min readJul 22, 2020

Kura Za Maoni CCM, Ushindi Kwa Demokrasia na Ushindi kwa Chama!

Kura za maoni CCM zilizo fanyika tarehe 20 na 21 July zimekua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku kila mtu akifuatilia michuano mbalimbali iliokua ikiendelea. Hata wanachama na viongozi wa vyama pinzani wameonekana kuvutiwa na kua na shauku kubwa ya matokeo mbalimbali yaliyo kua yakirushwa mubashara na vyombo vya habari.

Taratibu za upigaji kura mwaka huu ndani ya CCM imeonyesha jinsi chama hicho kikogwe kilivyo jikita kwenye uhuru na uwazi na demokrasia ya kweli. Wagombea wote wamepewa haki sawa za kujinadi na kura kupigwa na kuhesabiwa kwa uwazi mbele ya kadamnasi ya washiriki wote.

Matokeo ya demokrasia hii yameonekana kwa baadhi ya wabunge wa bunge la 11 na mawaziri wa awamu ya tano wakiangushwa kwenye kura za maoni. Tumeona Handeni Mjini mbunge aliemaliza muda wake Omary Kigoda akishika nafasi ya 4. Tumeona Kyera waziri Harrison Mwakyembe akishika nafasi ya 3. Na tumeona Kawe kijana Furaha Dominic Jacob akiwashinda watu maarufu kama Josephant Gwajima na Vincent Mashinji.

Hakika utaratibu wa mwaka huu umeondoa lawama na umewapa fursa watu ambao uwezo wanao na nia wanayo lakini huko nyuma walisita kuwania nafasi wakidhani ubunge ni wa watu fulani fulani tu. Kilicho baki sasa ni kwa kamati kuu kukaa na kuangalia sifa za ziada za wagombea na hatimai kupitisha wapeperusha bendera wa CCM kwa mwaka 2020.

Hakika utaratibu huu umezua gumzo mtaani na kwenye mitandao ya kijamii na kufanya macho na masikio ya Watanzania kwa siku mbili mfululizo zielekezwe CCM. Michuano mingi ilionyeshwa live na kurushwa na vyombo vya habari mbalimbali. Mpaka wanachama na viongozi mbalimbali wa upinzani wamekua waki tweet na kucomment mitandaoni kuliko hata wakati wa michakato ya ndani ya vyama vyao wenyewe. Wazungu wana ita hii “Must see TV”.

Ila mwisho wa yote, CCM imeweza kutumia mchakato wa kura za maoni kujinadi vyema kwa wananchi. Wananchi wameona mubashara jinsi demokrasia ndani ya chama inavyo fanya kazi na kwa hakika hii itashawishi watu zaidi kukipigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kwa hili Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu wa Uenezi wa CCM pamoja na waandaaji wote wa mchakato huu wanastahili pongezi.

Thomas J. Kibwana.

Thomas Joel Kibwana
Thomas Joel Kibwana

Written by Thomas Joel Kibwana

Political enthusiast. International Relations graduate. A fan of everything Tanzania.

No responses yet