Thomas Joel Kibwana
3 min readJun 29, 2020

Je Magufuli si Raisi Ambae Chadema Walikua Wakimtaka?

Wazungu huwa wana msemo wao, “Be careful what you wish for because you just might get it”, yani kua muangalifu na ukitamanicho kwa sababu unaweza ishia kukipata. Leo nataka nielezee ni kwa jinsi gani upinzani, haswa Chadema, kabla ya 2015,ilikua ikitamani raisi kama Magufuli labda pasipo hata wao kujua.

Tarehe 19 Juni, 2012, John Mnyika, wakati huo akiwa mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia Chadema alitoa kauli ifuatayo: Mimi nasikitishwa na jambo moja, tumefika hapa kutokana na udhaifu wa raisi Kikwete. Labda ndio maana Kikwete katiba hotuba yake ya kumkaribisha raisi mteule Magufuli mwaka 2015, akasema, “Naondoka mie, tumeleta chuma hiki…na mlikua mnasema mie mpole mpole, sasa mabadiliko kuleta mkali.” Raisi Kikwete alijua upinzani wa Tanzania ulikua unamchukuliaje na alijua anaekuja atakua tofauti na yeye kiutendaji. Sasa nitakua nimekosea nikisema Magufuli, asie na chembe za dalili za uzaifu ndio raisi Chadema walio kua wakimtaka kwa ajili ya Tanzania?

Hio hapo juu ni kauli ya kiongozi mkubwa wa Chadema ila sasa tudadavue kidogo ilani ya uchaguzi ya Chadema ya mwaka 2015. Ukrasa wa 9 inaelezea utendaji na uwajibikaji kwa watumishi wa umma ambapo Chadema ilisema ita tatua tatizo la poromoko la maadili kwa uongozi ambalo limesababisha omgezeko la “uzembe, rushwa, wizi, na ufisadi wa mali za umma miongoni mwa viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma.” Kwenye hili Magufuli katekeleza kwa asilimia kubwa kwa kupunguza watumishi hewa mwaka 2016, katika kufuma upya uongozi wa juu wa idara mbali mbali za serikali na kutumbua viongozi wa umma na wa kisiasa ambao wamekua wakikiuka miiko na maadali ya uongozi. Je huyu si raisi ambae Chadema walikua wakimtaka?

Tukiendelea na ilani hio hio ya Chadema.ya 2015, ukrasa wa 20 unaelezea jinsi watakavyo boresha sekta ya elimu ni pamoja na serikali kugharamia elimu kuanzia ya awali mpaka chuo kikuu na kutoa elimu bora. Je hivi havija fanywa na serikali ya awamu ya 5 chini ya raisi Magufuli? Je huyu si raisi ambae Chadema walikua wakimtaka?

Tukija ukurasa wa 25, inaelezea jinsi itakavyo boresha sekta ya afya kwa kuhamasisha Watanzania zaidi wajiunge na bima za afya za malipo nafuu na huduma kwa ajili ya wazee na wasio jiwezi. Raisi Magufuli alifumua na kuboresha bima ya afya pamoja na kufuta gharama za matibabu kwa wazee na wasio jiweza. Je huyu si raisi ambae Chadema walikua wakimtaka?

Kuhusu miundombini ambayo ni pamoja na reli, bandari, barabara na usafiri wa anga, kuanzia ukurasa wa 37 ilani ya Chadema ilisema itajenga reli mpya na kukarabati zilizopo kwa kiwango cha kisasa, kuboresha bandari zilizopo, kujenga barabara nchini haswa kijijini, kujenga shirika la ndege linalo jiendesha na kuboresha usafiri wa majini. Leo SGR ina jengwa, mfumo wa treni za umeme zina tengenezwa, barabara kiwango cha lami zimeongezeka, vivuko vimeboreshwa, meli mpya zimenunuliwa, bandari kulipo kua na rushwa na usisadi mkubwa kume boreshwa kiutendaji na shirika la ndege limefufuliwa. Jitihada zore hizi leo zina bezwa na upinzani ila zilikuepo kwenye ilani yao. Je huyu si raisi ambae Chadema walikua wakimtaka?

Hivyo ni baadhi ya vitu tu ambavyo vipo kwenye ilani ya uchaguzi wa 2015 wa Chadema na kuna vingine vingi kwa hio nakushauri ndugu msomaji uipitie ujionee mwenyewe jinsi awamu ya 5 inavyo tekeleza mipango mingi tu ambayo Chadema ilikua ikitilia kipaombele. Raisi Magufuli ni aina ya raisi waliemtaka na anatekeleza asilimia kubwa ya walivyo vitaka. Ndio maana ni nadra sana kwa viongozi wa Chadema kulinganisha ilani yao dhidi ya utendaji wa awamu hii. Kwa kuangalia vyote hivi, je huyu si raisi ambae Chadema walikua wakimtaka? Naomba utafakari hilo wakati tukielekea uchaguzi mkuu wa 2020.

Thomas J. Kibwana.

Thomas Joel Kibwana
Thomas Joel Kibwana

Written by Thomas Joel Kibwana

Political enthusiast. International Relations graduate. A fan of everything Tanzania.

No responses yet